Nafasi za kazi tuma maombi kabla ya tarehe 12 July 2019

Utangulizi
TODAYSKY COMPANY LIMITED , ni kampuni iliyosajiliwa na Mamlaka ya usajili wa biashara na leseni (BRELA) na kupewa namba 138-642-410. Kutoa huduma za uundaji wa mifumo (software development) na kutoa ushauri wa kitaalamu. Kampuni yetu inatengeneza mifumo ambayo inalenga kutatua changamoto zilizopo kwenye jamii hivyo kwa muda mwingi tunafanya kazi na jamii
Kampuni ya TODAYSKY inatoa fursa za ajira, hasa kwa wakazi wa Dodoma, Tuma maombi yako kwa baruapepe ajira@2daysky.com, kumbuka kuweka viambatanisho kama vyeti, CV, copy ya kitambulisho kama kipo, na barua ya kuomba kazi, Maombi yatumwe kati ya kada zifuatazo:-

 1. Afisa masoko

  Kampuni ya TODAYSKY inapenda kupata mtu atakayesimamia masuala ya masoko ya huduma zinazotolewa pamoja na miradi inayosimamiwa/kumilikiwa na kampuni.

  VIGEZO VYA KUZINGATIA

  1. Muombaji Awe na uwezo wa kusimamia shughuli za masuala ya masoko ya miradi inayomilikiwa na kampuni.
  2. Muombaji awe na uwezo wa kuwahudumia wateja kwa njia mbalimbali
  3. Muombaji awe na umri kati ya miaka 23-30
  4. Muombaji awe mhitimu wa elimu ya certificate/diploma katika kozi za biashara (Business administation/ sales/ Marketing)
  5. Muombaji awe anafahamu kutumia programu za compyuta

 2. Msimamizi wa mitandao ya kijamii

  Kampuni inahitaji muombaji ambaye ana uwezo mzuri na uzoefu katika kusimamia kurasa za mitandao ya kijamii, mwenye kutumia kugha nzuri katika uandishi na uongeaji.

  VIGEZO VY KUZINGATIA

  1. Muombaji awe na uwezo wa kuandika vizuri katika lugha ya kiswahili na kingereza
  2. Muombaji awe na elimu ya kuanzia kidato cha nne na kuendelea hadi diploma
  3. Mwombaji awe na umri kati ya miaka 19-29
  4. Muombaji awe na uwezo wa kutumia kompyuta
  5. Waombaji waliopitia shule/vyuo vya ufundi watapa kipaumbele zaidi
  6. Muombaji awe na uwezo wa kuongea vizuri na wateja (Customer care skills)

Je mwanafunzi wa chuo anaweza kufanya kazi nasi?

Kwa mwanafunzi unaweza kufanya kazi nasi kama intership, hivyo tuma maombi yako kupitia email ya ajira@2daysky.com, kumbuka kuambatanisha barua ya kuomba interniship, vyeti na nyaraka zinazoweza kuonyesha uzoefu wako,
Tuma maombi katika kada zifuatazo

 1. Masoko
 2. Huduma kwa wateja
 3. Uundaji wa mifumo (software development)
 4. Kubuni Graphics (Graphics design)